Marekani inaonesha kuwa iko tayari kuacha kutaja
hatua ya kijeshi katika azimio lolote la Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa kuhusu Syria.
Maafisa wa ikulu ya Marekani walisema
kumepatikana maendeleo katika juhudi za kupata azimio linalokubalika,
ambalo linaweza kujadiliwa baada ya ujumbe wa wakaguzi wa silaha za
kemikali wa Umoja wa Mataifa kutoa ripoti yao Jumatatu.
Mazungumzo baina ya Marekani na Urusi kuhusu
namna ya kudhibiti shehena ya silaha za kemikali za Syria yanaendelea
kwa siku ya tatu.
Huku nyuma, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban
ki-Moon, anasema anataraji kutafanywa duru ya pili ya mazungumzo ya
amani kuhusu Syria, mwezi ujao.
Akizungumza kwenye televisheni ya Ufaransa,
Bwana Ban alisema amezungumza na mjumbe wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu,
Lakhdar Brahimi kuhusu swala hilo hapo Ijumaa na wote wawili wanaona
hilo ni jambo muhimu.
0 comments:
Chapisha Maoni