Mtu mmoja amefariki papo hapo dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Noah alipokuwa akiendesha pikipiki huko katika kijiji cha Selewa, wilayani Mbozi katika mkoa wa Mbeya
Taarifa zinasema kwamba ajali hiyo imetokea jana baada ya gari lenye namba za usajili T. 535 BPN aina ya Toyota Noah lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Lameck Madihani, 45, Mkinga na mkazi wa Mlowo kumgonga marehemu aliyefahamika kwa jina la Baraka Kamwela, 24, Mndali na mkazi wa Mlowo na kusababisha kifo chake papo hapo.
Habari toka kwa maafisa wa polisi zinasema kuwa marehemu alikuwa na pikipiki aina ya yenye namba za usajili T.525 BTN lakini chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa na dereva aliyesababisha ajali hiyo tayari amekamatwa na gari lipo kituo cha polisi Mlowo huku taratibu zikifanywa ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.
Aidha kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa jeshi la polisi Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa madereva kuwa makini pindi watumiapo vyombo vya moto kwa kuzingatia sheria za usalama wa barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
0 comments:
Chapisha Maoni