Jumatatu, Agosti 12, 2013

UYOGA NI KINGA BORA DHIDI YA SARATANI

Virutubisho maalum vinavyopatikana kwenye uyoga, vimevuta hisia za watafiti kwa zaidi ya miaka 20 sasa ili kupata uhakika kwamba mboga hii ina uwezo mkubwa wa kutoa kinga kwa mwili wa mwanadamu dhidi ya ugonjwa wa saratani, ikiwemo ya matiti.

Uyoga una vitamini na aina nyingi za madini. Virutubisho vilivyothibitishwa kuwemo kwenye uyoga ni pamoja na Vitamin B2, B3, B5, B6, B Complex pamoja na madini ya Potasiamu na ‘phosphorus’. Virutubisho hivyo ni muhimu kwenye mwili wa binadamu katika kutoa na kuimarisha kinga ya kupambana na ‘wavamizi’ maradhi.
Aidha, inaelezwa kuwa uyoga ni chanzo kingine kizuri sana cha madini ya chuma (iron) na kopa ambayo yanahusika kwa kiasi kikubwa na uwezeshaji wa usambazaji wa hewa ya oksijeni mwilini. Kupatikana kwa madini ya chuma na kopa kwenye uyoga ni jambo la kipekee ambalo linafanya mmea huo kuwa tofauti na muhimu.

0 comments:

Chapisha Maoni