Mzee
wa miaka 70 amefariki dunia jana saa 6:30 usiku katika hospitali ya wilaya ya
Kyela mkoani Mbeya baada ya kupigwa na jiwe mbavuni.
Mzee
Aron Msole, 70, Mndali, Mkulima na mkazi wa kijiji cha Ibanda alikutwa na
umauti akiwa hospitalini kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kupigwa na jiwe
mbavuni na mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina la Anania Simtoe, 50,Mnyamwanga, mkulima
na mkazi wa Ibanda.
Chanzo
cha tukio hulo kimefahamika kuwa ni ng’ombe wa mtuhumiwa kuingia katika shamba
la marehemu na kuharibu mazao kitu kilichopelekea ugomvi uliosababisha mauti ya
marehemu. Mwili wa marehemu umekwisha fanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa
ndugu tayari kwa mazishi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya na kamishna
msaidizi wa jeshi la polisi Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na habari toka kwa maafisa wa polisi zinasema kuwa mtuhumiwa amekwisha
kamatwa na makachero wa polisi wakati taatibu za kumfikisha mahakamani
zikiendelea.
Pamoja
na hayo Kamanda Diwani Athumani ametoa wito kwa jamii kutatua matatizo au
migogoro yao kwa njia ya kukaa meza ya mazungumzo ili kuepuka
matatizoyanayoweza kuepukika.
0 comments:
Chapisha Maoni