Pichani juu ni taswira za ajali ya basi iliyouwa watu 41 na kujeruhi 33 katika eneo la Ntulele lililo kwenye mkoa wa bonde la ufa nchini Kenya.
Basi hilo lilikuwa likiwasafirisha zaidi ya abiria 60 kutoka mji mkuu wa Kenya, Nairobi kuelekea mji wa Homabay uliopo magharibi mwa Kenya lilikosa mwelekeo na kupinduka mara kadhaa usiku wa kuamkia Alhamisi.
Watu 33 walifariki papo hapo huku wengine 8 wakifariki baadaye walipokuwa wakipata matibabu hospitalini. Watu wengine 33 waliopata majeraha mabaya wanaendela kupata matibabu kwenye hospitali tofauti nchini Kenya.
Akituma rambirambi zake kwa familia za marehemu, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewataka madereva kuwa waangalifu na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kuhakikisha maisha ya Wakenya hayapotei kwa ajali za barabarani
0 comments:
Chapisha Maoni