WILAYA
YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 29.08.2013 MAJIRA YA SAA 18:30HRS HUKO KATIKA KJIJI CHA MWAPIMBUKA BARABARA YA
MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI
MKOA WA MBEYA. GARI T.877 CLX/T.242
CLV AINA YA IVECO LIKIENDESHWA NA HABIBU S/O HASSAN, MIAKA 28, MLUGURU,
MKAZI WA BUGURUNI DSM, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO PASTO D/O FURAHA, MIAKA 11, MNYIHA,MWANAFUNZI S/MSINGI IGURUSI
DARASA LA PILI MKAZI WA KIJIJI CHA MWAPIMBUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA CHAKE
WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA KITUO CHA AFYA IGURUSI. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA KITUO HICHO CHA AFYA. CHANZO MWENDO KASI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA KULITELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO MARA BAADA YA
AJALI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA
MOJA.
WILAYA
YA MBARALI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU
YA MOSHI
[GONGO] NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE.
[GONGO] NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE.
MNAMO TAREHE 29.08.2013 MAJIRA YA SAA 08:00HRS HUKO RUJEWA MJINI WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI
WAKIWA KATIKA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA EZEKIEL
S/O JAKOBO, MIAKA 26, MBENA,MKULIMA MKAZI WA UHAVILA NA WENZAKE SITA WAKIWA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO
WA LITA 25 PAMOJA NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO.
WATUHUMIWA NI WATUMIAJI NA WAUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI
WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA
MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
|
[ DIWANI
ATHUMANI – ACP ]
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Chapisha Maoni