Leo ni Jumanne tarehe 19 Shawwal 1434 Hijria sawa na 27 Agosti 2013.
Tarehe kama ya leo ya 27 Agosti mwaka 1806, yaani miaka 207 iliyopita, jengo la kihistoria mjini Zanzibar linalojulikana kwa jina la Beit al-Ajaib lililojengwa na Sultan Barghash bin Said huko Forodhani Unguja, liliteketezwa kwa mizinga ya manowari za Uingereza. Hatua hiyo ilifuatia ugomvi uliozuka baina ya wana wawili wa Kifalme. Watoto hao walijulikana kwa majina ya Said Barghash Khalid na Said Hamud bin Muhammad. Watoto hao wa Kifalme walikuwa wakigombana kukitawala kisiwa cha Zanzibar. Vita hivyo vilidumu kwa dakika 45 tu na kuwa vita vifupi zaidi duniani.
Siku kama ya leo miaka 1000 yaani tarehe 19 Shawwal 434 iliyopita alizaliwa Abu Zakaria Yahya bin Muhammad mashuhuri kwa jina la Ibn Mandeh ambaye alikuwa mwanahadithi, faqihi na mwanahistoria wa Kiirani. Alikuwa wa mwisho katika kizazi cha Ibn Mandeh na baada ya kupata elimu za zama zake alianza kufunza na kuandika vitabu. Mwanahistoria huyo wa Kiislamu ameandika vitabu vingi kikiwemo kile cha Maisha ya Tabarani.
Na katika siku kama ya leo miaka 22 iliyopita, yaani tarehe 27 Agosti mwaka 1991, nchi ya Moldova iliyoko mashariki mwa Ulaya ilipata uhuru. Kwa mujibu wa kumbukumbu za kihistoria nchi hiyo ilitawaliwa na kukaliwa kwa mabavu na tawala, kaumu na nchi mbalimbali zikiwemo, Ukraine, Russia, Romania na utawala wa Othmania. Baada ya mapinduzi ya kikomunisti nchini Russia, Moldova iliungana na Romania. Mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia, Moldova ilikaliwa kwa mabavu na Urusi. Hata hivyo baada ya kusambaratika Umoja wa Sovieti nchi hiyo ikajijitenga na kuwa uhuru.
0 comments:
Chapisha Maoni