WILAYA YA MBOZI – AJALI YA
GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO
NA KUSABABISHA KIFO
MNAMO
TAREHE 25/08/2013 MAJIRA YA SAA 09:30 HRS HUKO KIJIJI CHA CHIMBUYA WILAYA YA MBOZI. GARI NO 509 BNP/T 231 BME HORSE FAW
LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE RINGO S/O
SIJABAJE, MIAKA 34, MSAFWA NA MKAZI WA FOREST MBEYA, LILIMGONGA MTEMBEA KWA
MIGUU AITWAYE SAILOSI S/O CHEYO, MIAKA
14, MNDALI, MWANAFUNZI WA S/M CHIMBUYA DARASA LA SITA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE
PAPO HAPO, CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
KATIKA HOSPITALI YA WILAYA VWAWA.
DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVAKUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA
PIKIPIKI [BODABODA [KUGONGA GARI KWA
NYUMA NA KUSABABISHA KIFO.
MANMO TAREHE 25/08/2013 MAJIRA YA SAA 16:30 HRS HUKO MBALIZI MWAKAPANGALA WILAYA YA MBEYA
VIIJINI BARABARA YA TUNDUMA/MBEYA PIKIPIKI NO T.174 BSK AINA YA T/BETTER IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA
ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA MIAKA
20-25 ALILIGONGA KWA NYUMA GARI NO T. 388 BXS/T.183 ABX AINA YA SCANIA
SEMI TREILA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE JOSEPH S/O KISINDA, MIAKA 38, MHEHE
MKAZI WA DSM. MWENDESHA PIKIPIKI
ALIFARIKI WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI TEULE
YA IFISI, CHANZO CHA AJALI NI MWENDO
KASI WA MWENDESHA PIKIPIKI, DEREVA WA GARI AMERIPOTI NA GARI LIPO KITUONI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA MADEREVAKUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA
SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBOZI - AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI NA
KUSABABISHA KIFO.
KUSABABISHA KIFO.
MANMO TAREHE 25/08/2013
MAJIRA YA SAA 20:45HRS HUKO MAHENJE
BARABARA YA MBEYA /TUNDUMA GARI NO T. 561 BAJ AINA YA TOYOTA COSTER
LIKIENDESHA NA DEREVA BENARD S/O MLIMBA,
LILIMGONGA MPANDA BAISKELI AITWAYE FURAHA
S/O MWAIPOPO, MIAKA 26, MNYAKYUSA, DEREVA WA BODABODA NA KUSABABISHA KIFO
CHAKE PAPO HAPO NA KUMSABABISHIA MAJERAHA KWA ABIRIA AITWAYE NIONE S/O SANGA, MIAKA 27, MKINGA NA
MKAZI WA MWAKA TUNDUMA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA VWAWA NA MAJERUHI ANAPATIWA
MATIBABU HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA
MARA BAADA YA TUKIO HILO JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO
KWA MADEREVAKUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA
Signed by
[ DIWANI ATHUMANI
- ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Chapisha Maoni