TAARIFA YA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE”
TAREHE 24. 08. 2013.
WILAYA
YA MOMBA – WATU SABA WAKAMATWA KWA KOSA LA KUHARIBU MALI NA
KUJERUHI.
KUJERUHI.
MNAMO TAREHE 21.08.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MCHANGANI KIJIJI CHA SENGA KATA YA
KAMSAMBA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. KUNDI
LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KUTOKA KATIKA KIJIJI CHA ILAMBO KATA YA KAPETA WILAYA
YA SUMBAWANGA
VIJIJINI MKOA WA RUKWA WALIVAMIA MAKAMBI YA
WAVUVI YALIYOPO KATIKA KIJIJI HICHO NA KUWAPIGA KWA KUTUMIA FIMBO KISHA
KUCHOMA MOTO MABANDA KADHAA YA WAVUVI
YALIYOJENGWA KWA KUTUMIA NYASI.
CHANZO CHA TUKIO HILO NI KUGOMBEA
ENEO LA VIJIJI TAJWA. UFUATILIAJI WA MGOGORO HUU UNAENDELEA. JUMLA YA
WATU SITA WALIJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO AMBAO NI
1. MSABAHA S/O JUMA, MIAKA 40,
MZARAMO,MKULIMA/MVUVI 2. MAXIMO S/O MWAKANYEMBA, MIAKA
24,KYUSA,MKULIMA/MVUVI 3. MICHAEL S/O SANGA, MIAKA
30,MKINGA,MKULIMA/MVUVI 4. CHONDE S/O KALISTO, MIAKA 56,
MNYAMWANGA, MKULIMA/MVUVI 5. ZAWADI S/O
JOHN SICHULA, MIAKA 39, MNYAMWANGA, MKULIMA/MVUVI NA 6. GIBSON S/O EDWARD KACHINGWE, MIAKA 26, MSAGALA, MKULIMA/MVUVI
WAHANGA WOTE NI WAKAZI WA KIJIJI CHA
SENGA NA WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.
KUFUATIA TUKIO HILO JUMLA YA WATUHUMIWA
SABA WAMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI AMBAO NI 1. SAMWEL S/O DAUD, MIAKA 42,
MNYIHA, MKULIMA 2. GERVAS S/O LUKAS, MIAKA 52, MSUKUMA, MKULIMA 3.NYERERE S/O MWITA, MIAKA 52,MSUKUMA,MKULIMA 4.RICHARD S/O WILSON, MIAKA 43, MFIPA, MKULIMA 5. GEBRUS S/O RAMADHAN, MIAKA 28, MNYASA, MKULIMA 6. LULINDE S/O DASE, MIAKA 43, MSUKUMA,
MKULIMA NA 7. FUNGUZA S/O MASANJA,
MIAKA 43, MSUKUMA, MKULIMA WATUHUMIWA
WOTE NI WAKAZI WA KIJIJI CHA SENGA KAMSAMBA. KWA SASA HALI NI SALAMA KATIKA
ENEO HILO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII
KUTOJICHULIA SHERIA MKONONI NA KUITATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO. AIDHA ANATOA RAI KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA
MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WENGINE
WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.
WILAYA
YA KYELA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU
YA MOSHI [GONGO].
MNAMO TAREHE 23.08.2013 MAJIRA YA SAA 10:35HRS HUKO KYELA- KATI WILAYA YA KYELA
MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA KAMWELA S/O MWASAMWENE,MIAKA 37,KYUSA,MKULIMA,MKAZI WA MBUGANI
AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA NANE [08] AKIWA AMEBEBA KWENYE
BAISKELI YAKE. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA
YA MBEYA MJINI – KUINGIA NCHINI BILA
KIBALI.
MNAMO TAREHE
23.08.2013 MAJIRA YA SAA
17:30HRS HUKO UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA DEMARK S/O RAFOE,MIAKA 28,RAIA NA MKAZI
WA NCHINI ETHIOPIA AKIWA AMEINGIA
NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJII. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA
KUHUSU WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI HATUA ZA
KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
Signed by:
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Chapisha Maoni