Mtu mmoja amefariki dunia jana majira ya saa 11:30 alfajiri baada ya kugongwa na gari wakati akitembea kwa miguu huko wilayani Momba Mkoa wa Mbeya.
Maafisa wa polisi wamesema kuwa marehemu mwenye jinsi ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30-35 ambaye hajafahamika kwa jina wala anuani amekutwa na mauti papo hapo baada ya kugongwa na gari ambalo halijafahamika na dereva ambaye pia hajafahamika katika barabara ya Mbeya/Tunduma wilaya ya Momba mkoani Mbeya.

Habari zimeendelea kusema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika kituo cha afya Tunduma lakini dereva aliyesababisha tukio bado hajapatikana kwani alitoroka baada tu ya kusababisha ajali.
Pamoja na hayo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya na Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi Diwani Athumani ametoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto kwa kuzingatia sheria za usalama wa barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa juu ya mahali alipo mtuhumiwa azitoe katika mamlaka husika ili chukuliwe sheria.
0 comments:
Chapisha Maoni