Mtu mmoja amefariki dunia na 15 wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Hood likitokea kilombero kwenda jijini Dar es salaam kumgonga mtembea kwa miguu na kisha kuacha njia na kupinduka katika eneo la Kiembeni Mikese Mkoani Morogoro.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro Bonifasi Mbao akizungumza kwenye eneo la tukio amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi gari ilimshinda na kugonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka ambapo dereva wa basi amekimbia mara baada ya tukio la ajali Taarifa za madaktari katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro zimeeleza majeruhi wanaendelea na matibabu na mwili wa marehemu umehifahiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa morogoro .
0 comments:
Chapisha Maoni