WILAYA YA MBARALI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
|
MNAMO TAREHE 21.08.2013 MAJIRA YA SAA 13:45 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MLANGALI WILAYA YA MBARALI MKOA WA
MBEYA. GARI T.901 ASQ/T.415 AXA AINA
YA SCANIA
LIKIENDESHWA NA DEREVA SHADRACK S/O
HAMIS, MIAKA 34, MMAKUA, MKAZI WA IRINGA LIKITOKEA MBEYA KUELEKEA MAFINGA
LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MONICA D/O
MHAHWA, MIAKA 56, MBENA, MKAZI WA MAKETE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE MUDA
MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA KATIKA
HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA
AMEKAMATWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI HIYO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA
SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
[ DIWANI
ATHUMANI – ACP ]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Chapisha Maoni