Jumatatu, Mei 15, 2017

USD 39,000 BANDIA ZAKAMATWA MBEYA

Siku ya juzi majira ya saa 10:00 Asubuhi, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako katika Kitongoji cha Mapelele kilichopo Kata ya Mtengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kuwakamata Nobat Mushi (23), Takeshi Nundo (27) na Hemed Msangi (26) ambao wote ni wakazi wa Forest, mkoani Mbeya.
Watuhumiwa kwa pamoja walikamatwa wakiwa na dola bandia noti 390 kila moja ikiwa na thamani ya dola 100, kama dola hizo zingekuwa halali zingelikuwa na thamani ya dola 39,000 ambayo ni sawa na pesa za kitanzania shilingi 85,800,000. 
Watuhumiwa walikamatwa na fedha hizo ambazo walikuwa wamezihifadhi kwenye mkoba na kuziweka ndani ya gari yenye namba za usajili T.715 aina ya Altezza.
Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

0 comments:

Chapisha Maoni