Jumapili, Machi 19, 2017

ZANZIBAR KUTOKATIWA UMEME

Rais Magufuli leo tarehe 19 Machi 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Ikulu Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Kahitwa Bishaija na Meneja Mwandamizi wa Fedha wa TANESCO Bw. Sadock Mugendi.
Wakati huo huo, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amewatoa hofu wananchi wa Zanzibar kuwa hawatakatiwa umeme baada ya Serikali ya Mapinduzi (SMZ) kuanza kulipa deni inalodaiwa na TANESCO.
Prof. Muhongo amesema tayari SMZ imeanza kulipa kiasi cha Shilingi Bilioni 10 na itaendelea kulipa deni hilo mpaka litakapomalizika.
Aidha, Prof. Muhongo ametoa wito kwa wadaiwa sugu wote wa TANESCO kulipa madeni yao katika kipindi cha siku 5 zilizobaki kwa kuwa wasipolipwa watakatiwa umeme.

0 comments:

Chapisha Maoni