Jumamosi, Machi 18, 2017

TUNDU LISSU RAIS TLS!

Taarifa kutoka jijini Arusha ambako uchaguzi wa rais ndani ya TLS (Tanganyika Legal Society) ulikuwa ukifanyika leo ni kuwa Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Antipas Lissu amepata ushindi wa kishindo wa 88%.
Mwanasheria mkuu huyo wa Chadema Tundu Lissu achaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika kwa jumla ya kura 1,411 kati ya 1,682 zilizopigwa.

0 comments:

Chapisha Maoni