Ijumaa, Machi 24, 2017

SHEHENA YA POMBE HARAMU (VIROBA) YAKAMATWA MBEYA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. 
Kufuatia mapambano yanayoendelea nchi nzima dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa Pombe kali zilizopigwa marufuku [viroba], Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya misako na operesheni katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya ambayo ni Uyole, Kabwe, Sae, Mwanjelwa Jijini Mbeya, Kyela kati, Kalumbulu – Kyela, Ngyekye – Kyela, Rujewa – Mbarali na Kibaoni - Chunya na kufanikiwa kukamata watu [wafanyabiashara] wakiwa na Pombe kali zilizopigwa marufuku [Viroba] pamoja na watumiaji wa pombe hizo. 

Katika Operesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 09 ambao pia ni wafanyabiashara walikamatwa wakiwa na Pombe Kali zilizopigwa marufuku [viroba] ambao ni:-
1. OBEDI NYARUKE [50] Mkazi wa Uyole Jijini Mbeya.
2. MARTIN MAKWAYA [29] Mkazi wa Kyela
3. NETO MWAKAJILA [38] Mkazi wa Kalumbulu Kyela
4. MTULEKE EMANUEL [40] Mkazi wa Ngyekye Kyela
5. ERASMO DANDA [50] Mkazi wa Ihanga Mbarali
6. JOYCE BATHLOMEO [36] Mkazi wa Kibaoni Chunya
7. NESTORY FILBERT [23] Mkazi wa Lupatingatinga – Chunya
8. FILBERT KALUMANZILA [60] Mkazi wa Makongolosi Chunya 
9. JOSHUA MWAKAJA [42] Mkazi wa Makongolosi Chunya

Katika Operesheni hiyo jumla ya katoni 105 za Pombe kali aina ya Konyagi [viroba original] zilikamatwa na paketi 106 za Konyagi [viroba original]. Pia zilikamatwa pombe kali zilizopigwa marufuku aina mbalimbali ambazo ni value auter katoni 14, viroba aina ya “high life” paketi 180, Fiesta paketi 450, [viroba] paketi 340 aina ya ridder, gun paketi 165 na chupa za ridder 60 na paketi 9,840 aina ya Shujaa.
Aidha mnamo tarehe 20.03.2017 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilipokea taarifa toka kwa WITNESS DAMAS TESHA [34] Mfanyabiashara na Mkazi wa Sae ambaye alikuwa na lengo la kusalimisha Pombe kali zilizopigwa marufuku ambazo zilikuwa zimehifadhiwa kwenye Stoo yake ya Vinywaji. Kutokana na taarifa hiyo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa [TFDA] walifika eneo la Sae, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga na kufanya upekuzi katika Stoo ya Vinywaji na Vyakula inayomilikiwa na WITNESS DAMAS TESHA [34] na kukuta amehifadhi pombe kali aina mbalimbali kama ifuatavyo:-

i. Kiroba kikubwa katoni 55 [12 * 12] mils 100
ii. Kiroba kidogo katoni 25    [ 12 *12] mils 50
iii. Fiesta ndogo katoni 64 [15 *15} mils 50
iv. Nguvu kubwa katoni 26 [12 *12] mils 100
v. Konyagi viroba katoni 184 mils 50 @ 144
vi. Konyagi kubwa viroba katoni 25 mils 100 @ 144
vii. Konyagi katoni 65 mils 100 @ 100
viii. Konyagi kubwa katoni 44 mils @ 240
ix. Valeur kubwa katoni 40 mils @ 144
x. Valeur ndogo katoni 26 mils 50 @ 240
Jumla ya katoni zote ni 454.

Mnamo tarehe 23.03.2017 majira ya saa 08:00 asubuhi Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilipokea taarifa toka TBL Tawi la Mbeya @ Kwa Ndiyo ambazo zilikuwa na lengo la kusalimisha Shehena ya Pombe kali [viroba] zilizokuwa zimehifadhi katika Bohari lililopo Kata na Tarafa ya Iyunga jijini Mbeya. Kutokana na taarifa hizo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa [TFDA] walifika katika Bohari hiyo ya Vinywaji inayomilikiwa na TBL Tawi la Mbeya na kufanikiwa kukuta shehena kubwa ya Pombe kali [viroba] zilizopigwa marufuku za aina mbalimbali kama ifuatavyo:-

i. Konyagi pesheni [144 x 90] katoni 187 
ii. Konyagi Gin [20x50] katoni 5 
iii. Konyagi Gin [144x50] katoni 1,855 
iv. Konyagi Gin [240x50] katoni 10 
v. Konyagi Gin [1x100] katoni 3 
vi. Kongagi Gin [100x100] katoni 3,729 
vii. Konyagi Ukwaju [144x90] katoni 32 
viii. Vladimir Vodka [144x100] katoni 89 
ix. Bongo bond [240 x50] katoni 102 
x. Vladimir Vodka katoni 108 
xi. Bismark Rock [180 x 50] katoni 4 
xii. Bismark Rock [15x50] katoni 7 
xiii. Regency Whisky [240 x 50] katoni 105 
xiv. Zanzi choclolate [96x90] katoni 58 
xv. Zanzi cream [96x90] katoni 58 
xvi. Valuer [20x50] katoni 4 
xvii. Valuer [240x50] katoni 3008 
xviii. Regency whisky [144x100] katoni 16 
xix. Valuer [12x100] katoni 5 
xx. Valuer [144x100] katoni 1,527 

Jumla ya katoni zote ni 10,993 mali ya Tanzania Distillers LTD.

Aidha mnamo tarehe 23.03.2017 majira ya saa 13:30 mchana huko eneo la Mbalizi stendi ya zamani, Kata ya Songwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na kikosi kazi kilichoshirikisha Maafisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa [TFDA] na Maafisa wa NEMC na Afisa Afya walimkamata AMBAKISYE MWAMPEJELE [50] Mfanyabiashara na Mkazi wa Mbalizi akiwa na pombe kali zilizopigwa marufuku na Serikali zikiwa katika vifungashio vya plastiki kama ifuatavyo:- 
i. Ridder Tanzania dazani 20 [20x20] mil 100 
ii. Ridder Tanzania paketi 17 mil 50
iii. Konyagi ukwaju katoni 1 mil 90
iv. Konyagi viroba katoni 2 mil 90
v. Konyagi viroba katoni 1 mil 50
vi. Burudani viroba wine paketi 60  mil 200
vii. Burudani viroba wine paketi 118 mil 150
viii. Boss viroba paketi 96 mil 100
ix. Boss viroba paketi 260 mil 50
x. Nguvu viroba paketi 24 mil 100
xi. Regence viroba paketi 40 mil 50
xii. Bongo bond whisky paketi 60 mil 50
xiii. Vladimir vodka viroba paketi 23 mil 50
xiv. Valuer viroba paketi 20 mils 50
xv. Necha viroba paketi 12 mil 100
xvi. Zanzi viroba paketi 3 mil 100
xvii. Konyagi viroba paketi 89 mil 100
xviii. Konyagi viroba paketi 24 mil 50
xix. Premium vodka viroba paketi 60 mil 100
xx. Konyagi viroba katoni 3 mil 100 na 
xxi. Konyagi viroba katoni 5 mil 50.

Jumla ya katoni zote ni 32 na Paketi 906

Hadi kufikia tarehe 24.03.2017 jumla ya Katoni 11,598 na Paketi 11,987 za Pombe Kali zilizopigwa marufuku na Serikali zikiwa katika vifungashio vya plastiki [viroba] zimekamatwa.

0 comments:

Chapisha Maoni