Jumanne, Machi 07, 2017

RIPOTI INAONESHA SASA WANAWAKE WANAUNGWA MKONO ZAIDI KUFANYA KAZI NJE YA NYUMBA ZAO

Shirika la kazi la kimataifa ILO leo huko Geneva limetoa ripoti, ikionesha kuwa watu wengi zaidi wanaunga mkono wanawake kufanya kazi nje ya nyumba.
Ripoti hiyo iliyoandaliwa na ILO kwa kushirikana na kampuni ya Gullup inaonyesha kuwa, asilimia 70 ya wanawake na asilimia 66 ya wanaume kati ya wahojiwa laki 1.5 katika nchi na sehemu 142 duniani, wanaunga mkono wanawake kufanya kazi zenye mapato nje ya nyumba.
Ripoti pia inaonyesha kuwa, wanawake na wanaume wenye kiwango cha juu cha elimu wanapenda zaidi wanawake kufanya kazi nje na kutunza familia kwa wakati moja.

0 comments:

Chapisha Maoni