Ijumaa, Machi 31, 2017

MANISPAA YA IRINGA KUTUMIA BILIONI 1.3 KUTENGENEZA BARABARA


Mamlaka ya Manispaa ya Iringa ijumaa ya leo leo imetia saini mikataba yenye gharama ya shilingi bilioni 1.3 za kitanzania kwaajili ya matengenezo ya barabara  za ndani ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kupitia fedha za mfuko wa barabara.  
Mikataba hiyo imesainiwa na Meya wa Manispaa ya Iringa mheshimiwa Alex Kimbe (Chadema) ambaye amewataka wakandarasi hao kufanya kazi kwa bidii na kwa wakati waliokubaliana ikiwa ni pamoja na kushirikisha jamii ya watu inayowazunguka.  
Jumla ya wakandarasi 14 walikidhi vigezo vya zabuni hizo ambapo kazi zitakazofanyika ni kutengeneza barabara, madaraja na mifereji ya maji ya mvua ndani ya Manispaa.

0 comments:

Chapisha Maoni