Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema
kuwa televisheni ya CNN ya Marekani imekuwa chombo cha kueneza
propaganda za kisaisa za nchi hiyo.
Maria Zakharova amekosoa habari za kichochezi zinazotangazwa na
televisheni ya CNN ya Marekani na kusema yanayojiri Marekani yanaonesha
jinsi vyombo vya habari vinavyoshiriki katika michezo ya kisaisa,
mashinikizo na kutoa vitisho.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameongeza kuwa,
televisheni ya CNN ilipoteza hadhi na uaminifu wake mbele ya walimwengu
muda mrefu uliopita.
Kuhusu madai ya televisheni ya CNN kwamba Rais Vladmir Putini
aliafikiana na Donald Trump juu ya kutoa pigo dhidi ya Hillary Clinton
katika uchaguzi uliopita wa Rais wa Marekani, Maria Zakharova amesema
kuwa, katika kampeni zake za uchaguzi, mgombea aliyeshindwa wa chama cha
Democratic alisema: Inasikitisha kuona kwamba CNN imebadilika na kuwa
chombo kilichochuja.
Televisheni ya CNN ambayo katika kipindi cha kampeni za uchaguzi wa Rais
wa Marekani ilituhumiwa kumuunga mkono na kumpigia debe Hillary
Clinton, imekuwa ikimkosoa vikali Rais wa sasa wa nchi hiyo, Donald
Trump na kumtuhumu kwamba alikuwa na uhusiano na ushirikiano wa siri na
Rais Vladmir Putin wa Russia.
0 comments:
Chapisha Maoni