Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya juzi lilifanya misako katika maeneo mbalimbali dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya. Katika misako hiyo watuhumiwa 03 walikamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi.
Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
1. MALONGO SOLO [25] Mkazi wa Hapoloto – Mbalizi
2. MATHA DICKSON [20] Mkazi wa mtaa wa Magereza – Rungwe
3. AMON MWAKAJONGA [30] Mkazi wa kitongoji cha Kilambo – Kyela
Katika misako hiyo, watuhumiwa walikamatwa wakiwa na Bhangi yenye uzito wa Kilogram 06 na gram 20 ikiwa imehifadhiwa kwenye mfuko wa sandarusi na mfuko wa Rambo. Watuhumiwa ni wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika, taratibu za kuwafikisha mahakamani zitafuata.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuwafichua wahalifu na mtandao wa wahalifu wanaojihusisha na biashara ya Pombe kali zilizopigwa marufuku pamoja na dawa za kulevya ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Aidha Kamanda KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kufanya kazi na kuacha kujihusisha na biashara ya Pombe Kali zilizopigwa marufuku [viroba] pamoja na uhalifu kwa ujumla kwani Jeshi la Polisi halitavumilia aina yoyote ya uhalifu.
0 comments:
Chapisha Maoni