Ijumaa, Machi 24, 2017

AZAM FC WAJIANDAA KUWAKABILI YANGA

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, jioni ya jana ilianza rasmi mazoezi ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Yanga.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utafanyika Aprili Mosi mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi hicho kimeanza mazoezi huku kikiwakosa nyota wake saba waliokuwa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, ambao ni kipa Aishi Manula, mabeki Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Gadiel Michael.
Viungo ni Nahodha Msaidizi Himid Mao, Frank Domayo na Salum Abubakar, ambao wanajiandaa na mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Botswana (Machi 25) na Burundi (Machi 28).
Mara ya mwisho Azam FC kukutana na Yanga, ilikuwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, ilipopata ushindi wa kihistoria dhidi ya wanajangwani hao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.
Katika mchezo wa raundi ya kwanza ya ligi, timu hizo zilitoka suluhu huku ikishuhudiwa Azam FC ikitawala mchezo na kukosa nafasi nyingi za kufunga mabao.
Akizungumza Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, alisema kuwa vijana wake wamerejea mazoezi wakiwa na ari nzuri baada ya mapumziko ya siku mbili.

0 comments:

Chapisha Maoni