Ijumaa, Februari 24, 2017

RIHANNA ATAMBA, AMFICHA MICHAEL JACKSON

Rihanna amempiku Michael Jackson katika kuwa na nyimbo katika chati ya nyimbo kumi bora nchini Marekani.
Hii ni baada ya wimbo wake mpya wa Love on the Brain kuingia kwenye orodha hiyo.
Wimbo huo ni wake wa 30 kuwa kwenye chati hiyo, na sasa ameachwa nyuma na The Beatles na Madonna pekee.
Madonna ana nyimbo 38 zilizowahi kuwa kwenye chati hiyo. The Beatles wana nyimbo 34.
Majina mashuhuri zaidi ya watoto
Beyonce atawala tuzo za MTV Marekani
Jackson, aliyefariki Juni 2009, alikuwa na nyimbo 29 katika chati hiyo ya nyimbo kumi bora.
Mwaka 2005, wimbo wa Rihanna wa Pon De Replay ulikuwa namba mbili katika chati za muziki Marekani na Uingereza.
Imemchukua miaka 10, miezi saba na wiki mbili kuwa na nyimbo 30 kwenye chati ya nyimbo bora Marekani.
Nyimbo zilizovuma za Madonna alizichomoa katika kipindi cha miaka 13.
Rihanna alimfikia Madonna orodha ya waimbaji wa kike wenye nyimbo nyingi zaidi chati ya 100 bora Marekani Julai 2016
The Beatles walifika hapo kwa kutumia miaka mitano, miezi tisa na wiki mbili pekee.

0 comments:

Chapisha Maoni