Rais wa Jamhuri ya Uganda. Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili.
Amepokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Mapokezi yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
0 comments:
Chapisha Maoni