Aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, SACP Ahmed Msangi jioni ya leo ameagana na wanambeya pamoja na staff nzima ya Redio Mbeya Fm ya jijini Mbeya kupitia kipindi cha TABARADI na kueleza tathmini ya ya kazi aliyoifanya kwa kipindi cha miaka miwili na miezi mitatu.
Kamanda huyo ameeleza kuwa uhamisho wake kwenda mkoani Mwanza ni wa kawaida kwa jeshi la polisi Tanzania ambapo anabadiliwa na aliyekuwa kamanda wa polisi mkoani Mwanza ACP Justus Kamugisha .
Kutoka kushoto ni wafanyakazi wa Mbeya fm: Yohana Mwambene (Mwandishi wa FICHUO BLOG), David Nyembe, Anangisye Essau, Kamanda Ahmed Msangi (mwenye bluu), Gwamaka Mwankota na Fredy Jackson |
Ahmed Msangi ameeleza kuwa kati ya changamoto kubwa kwa jeshi la polisi katika kipindi chake alichohudumu kama kamanda wa polisi ni matatizo ya raia kujichukulia sheria mkononi na kusababisha mauti kwa watuhumiwa wa makosa mbalimbali ambapo kwa mkoa wa Mbeya matukio hayo hujitokeza mara kwa mara kwa watu wanahisiwa kuwa ni washirikina, wezi na majambazi na makundi mengineyo.
Pamoja na hayo kamabda Ahmed Msangi anaingia katika kumbukumbu ya kuwa kati ya makamanda wa polisi wa mikoa waliofanikiwa kujenga ushirikiano mzuri na wananchi na kufanikisha kupambana vema na changamoto za usafirishaji/matumizi ya madawa ya kulevya na bidhaa za magendo,uhamiaji haramu,uhujumu nyara za serikali,upigwaji wa nondo na pombe haramu pamoja na mengi.
Pamoja na hayo amewashukuru wakazi wa Mbeya waliotoa ushirikiano kwa jeshi la polisi katika kipindi chote, vyombo vya habari na idara mbalimbali na kisha ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Mbeya kuupenda mkoa wao, kushiriki vema katika kuulinda kwa namna zote na kushirikiana na vyombo vya dola ili kuumbua uhalifu katika jamii na pia amewataka kutoa ushirikiano na kamanda mpya wa polisi mkoa wa Mbeya, ACP Justus Kamugisha kwani anaamini ataweza kufanya kazi vema pengine hata kushinda yeye.
SACP Ahmed Msangi alianza kuhudumu kama kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya mwishoni mwa mwaka 2013 baada ya kamanda aliyekuwepo Diwani Athumani kuhamishiwa makao makuu. FICHUO BLOG na Mbeya fm Radio inamshukuru kwa ushirikiano wake katika kipindi chote alipokuwa akihudumu kama kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya.
0 comments:
Chapisha Maoni