Wabunge nchini Ufaransa wamepitisha
mswada ambao unaharamisha watu kulipa ili kupata huduma ya ngono na
kuweka faini ya hadi dola 4,274 kwa wale watakaopatikana na hatia.
Wale
watakaopatikana na hatia pia watalazimika kupewa mafunzo ya mazingira
yanayowakabili makahaba.Imechukua zaidi ya miaka miaka miwili kupitisha
mswada huo wenye utata kutokana na tofauti zilizopo kati ya mabunge
mawili kuhusu swala hilo.
Baadhi ya makahaba waliipinga sheria hiyo wakati wa mjadala wa mwisho.
Waandamanaji
60 walipiga kambi nje ya bunge mjini Paris, walibeba mabango moja
likiwa na maandishi yaliosema:''Sina haja ya kukombolewa, nitajikomboa
mwenyewe'',kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Muungano wa makahaba wa Strass umesema kuwa hatua hiyo itaathiri
maisha ya kawaida ya makahaba wanaodaiwa kuwa kati ya 30,000 na 40,000.
Lakini wanaounga mkono sheria hiyo wanasema itasaidia kukabiliana na mitandao ya ulanguzi wa binaadamu.
Pia
itakuwa rahisi kwa makahaba wa kigeni kupata kibali cha kufanyia kazi
kwa mda nchini Ufaransa iwapo watakubali kutafuta kazi zisizo za
ukahaba.
Umuhimu wa sheria hiyo ni kushirikiana na makahaba ,kuwapatia vibali vya
utambuzi kwa sababu tunajua asilimia 85 ya makahaba ni waathiriwa wa
ulanguzi wa binaadamu ,mbunge wa chama cha kisosholisti Maud Oliver
ambaye alifadhili sheria hiyo aliambia chombo cha habari cha AP.
0 comments:
Chapisha Maoni