Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 80 amekutwa akiwa amefariki ndani ya choo cha msikiti wa Ibadhi ulioko Bopwe karibu na Ofisi za Baraza la Wawakilishi Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini Kwake , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Kamishina msaidizi Hassan Nassir Ali alisema aliyefikwa na mauti hayo ni Hassan Ali Juma mkaazi wa Bopwe Wete .
Alisema mzee huyo aliondoka nyumbane kwake machi 9 majira ya saa saba , kuelekea msikitini kwa ajili ya maandalizi ya swala ya adhuhuri , na kuonekana machi 10 majira ya saa 12.45 jioni akiwa amefariki ndani ya choo .
Inadaiwa kuwa mzee huyo baada ya kufika msikitini aliingia chooni kisha kufunga mlango kwa ndani ambapo alianguka akiwa katika harakati za kufua fulana alilokuwa amevaa ili aoge.
0 comments:
Chapisha Maoni