Matokeo ya mtihani wa taifa wa Kenya KCSE uliofanyika mwaka jana yametolewa. Matokeo yanaonyesha kuwa ni theluthi moja tu ya wanafunzi zaidi ya laki 5.2 waliofanya mtihani huo wamefikisha alama zinazowaruhusu kujiuonga na vyuo vikuu.Waziri wa Elimu wa Kenya Dk Fred Matiang'i ameonyesha wasiwasi kuhusu idadi ndogo ya wanafunzi ambayo watajiunga na chuo kikuu, Baadhi ya wakenya wameanza kujiuliza kuhusu elimu nchini Kenya, na kama mazingira ya elimu yaliyopo sasa yanasaidia au yanakwamisha elimu.




0 comments:
Chapisha Maoni