Chuo kikuu cha Imperial cha Uingereza kimetoa ripoti ikionesha kuwa
kelele za kudumu zinazoletwa na mawasiliano ya barabara zinaweza
kuathiri muda wa maisha ya binadamu.
Watafiti wa chuo kikuu cha Imperial na chuo kikuu cha London walichunguza na kulinganisha takwimu za afya za wakazi milioni 8.6 wa London kuanzia mwaka 2003 hadi 2010 na kiwango cha kelele za barabara katika sehemu nyingi za mji huo. Katika kipindi hicho, watu wazima laki 4.4 walifariki kutokana na vyanzo mbalimbali.
Watafiti waligundua kuwa, kiwango cha vifo cha watu wazima wenye umri zaidi ya miaka 25 na wazee wenye umri zaidi ya 75 wanaokaa katika shemu zenye kelele za barabara zaidi ya 60 db ni asilimia 104 ya wale wanaoishi katika sehemu kimya.
Watafiti wamesema, vifo hivi vinahusiana na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, chanzo chao kinaweza kuwa kelele zilizosababisha kupanda kwa shinikizo la damu, ukosefu wa kulala na shinikizo la akili.
Watafiti wamesema, ingawa hivi sasa haiwezi kutambua kama kelele ina athari kubwa zaidi kuliko tabia za kula, uvutaji wa sigara na ukosefu wa mazoezi, lakini utafiti huo una maana yake na utafiti mwingi zaidi unahitajika kufanywa katika sekta hiyo.

sasa kwa namna hiyo tufanyeje maana mimi ni dereva kutwa nzima niko kwenye gari halafu kelele
JibuFuta