Saratani ya Kongosho ni saratani kali sana ambayo inasababisha asilimia 90 ya vifo vya watu. Mzinduzi wa Kampuni ya Apple Steve Jobs alifariki kutokana na saratani hiyo ambayo inadhaniwa kuhusiana na uvutaji sigara, unene, na ugonjwa wa kisukari.
Watafiti wa kituo cha utafiti wa saratani cha Japani wamegundua kuwa mafuta aina ya n-3 yanayopatikana kwenye samaki yanaweza kupunguza hatari ya saratani ya kongosho, kwa sababu yanaweza kupunguza uvimbe wa kongosho.
Watafiti wa kituo hicho walichunguza takwimu za afya za watu elfu 82, wakagundua kiwango cha kupata saratani ya kongosho kwa watu wanaotumia mafuta ya samaki aina ya n-3 ni asilimia 70 ya kile cha watu wasiotumia mafuta hayo.
0 comments:
Chapisha Maoni