Alhamisi, Februari 25, 2016

KAYA 231 ZINAISHI KWA KULA MATUNDA YA PORINI LINDI

Hekari zaidi ya 545 za mahindi na mpunga zilizoko katika kijiji cha Nanjulu tarafa ya mandawa wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi zimesombwa na maji kufuatia mafuriko yaliyo sababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo kaya 231 zinaishi katika maisha ya shida na kula matunda ya porini kama chakula cha kuwafanya waendelee kuishi.
Nihali isiyo ya kawaida kwa wahanga hao baada ya mtafiti wa kituo cha utafiti wa mazao jamii ya mizizi cha naliendele kutoa sampu ya shina la Mhogo kwa mkuu wa wilaya ya Ruangwa Bi.Mariamu Mtima nakuamua kuwapa akina mama moja na jingine akina baba wagawane matarajio yake yalikatishwa ghafla na kile kilicho daiwa kuwa ni njaa na kuanza kunyang’anyana Mhogo huo ambapo wameiomba serikali kuwatazama kwa jicho la tatu kwani maisha yao yamekuwa wakiishi kwa kula matunda ya porini.
Wahanga hao wakiwemo viongozi wa taasisi ya utafiti na maendeleo naliendele wametembelea maeneo yalipo kuwa mashamba hao nakukuta mazao yamesombwa na maji ambapo mratibu mazao jamii ya mizizi kitaifa Daktari Geoffrey Mkamilo amesema imewalazimu kupeleka mbegu hizo zinazozaa kwa muda mfupi ili wahanga hao wapate kujikwamua kimaisha baada ya miezi miwili ijayo kuanzia sasa.
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Bi.Mariamu Mtima akipokea mbegu hizo ameshukuru kituo cha mbegu cha naliendele kwa kutoa mbegu hizo ambazo zitawafanya wahanga hao kurudi katika hali ya kupata chakula kwa muda mfupi sambamba na kuwataka vijana waache kucheza pulu na bao badale yake walime iliwaondokane na umasikini.

0 comments:

Chapisha Maoni