Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe ameilalamikia serikali ya Magufuli kwa kitendo chake cha kukaa kimya kuhusu ufisadi unaoendelea kufanywa na Harbinder Singh Seth, mmiliki wa IPTL, ambaye huvuna kiasi cha malipo ya bilioni 4 kila mwezi kama malipo ya kuliuzia umeme shirika la ugavi wa umeme nchini, Tanesco.
Zitto ambaye ni mmoja wa wabunge walioibua na kusimamia kidete sakata la ufisadi wa Tegeta Escrow bungeni mwishoni mwa mwaka juzi (2014), amesema hayo kufuatia tangazo la serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import Support ya miaka ya miaka 1980 na 1990s, ambapo ameisifu serikali kwa hatua hiyo na kuhoji iweje ikomae na kashfa hiyo tu, huku ikisita kuchukua hatua kwenye sakata la IPTL linaloigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha kila mwezi isivyostahili?
Kampuni ya IPTL imeshalipwa fedha mara mbili tangu Rais Magufuli aingie rasmi madarakani, hivyo kufanya hesabu zitimie bilioni 8 kwa kipindi cha miezi miwili mpaka sasa.
Msome;
"Nimeona tangazo la Serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import Support. Hii ni kashfa ya miaka ya 1980s na 1990s. Ni hatua nzuri. Lakini ina maana gani wakati Serikali inavuta miguu kwenye suala la IPTL? Harbinder Singh Seth na genge lake wanavuta tshs 4bn kila mwezi. Kwa kutochukua hatua kuhusu IPTL, Rais Magufuli ameshaipotezea nchi mapato ya tshs 8bn tangu aingie madarakani. #TegetaEscrow ndio baba la mtandao wa ufisadi nchini kwetu"
Zitto Kabwe.
0 comments:
Chapisha Maoni