Ripoti iliyotolewa hivi karibuni imeonesha kuwa watoto milioni 30 katika nchi zilizostawi duniani wanaishi katika umaskini.
Ripoti iliyotolewa na taasisi ya Save the Children imesema watoto milioni 570 duniani wanaishi katika umaskini wa kupindukia na wengine milioni 950 wanakabiliwa na hatari ya umaskini.
Ripoti ya taasisi ya Save the Children imesema kuwa watoto milioni 30 wanaoishi katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano na Kiuchumi na Ustawi wanasumbuliwa na umaskini wa namna moja au nyingine. Imeongeza kuwa asilimia 27 ya watoto hao katika nchi za Umoja wa Ulaya wanakabiliwa na hatari ya umaskini na dhulma za kijamii.
Ripoti ya Save the Children imeonesha kuwa, asilimia 73 ya watu maskini duniani wanaishi katika nchi zenye pato la wastani. Imetilia mkazo kwamba umaskini baina ya watoto una mfungamano mkubwa na dhulma za kijamii na kiuchumi na unakita mizizi zaidi kutokana na ukosefu wa usawa wa kimuundo na wa kisiasa katika nchi mbalimbali.
0 comments:
Chapisha Maoni