Jumatano, Januari 20, 2016

VYAKULA JAMII YA KARANGA HUREFUSHA MAISHA

Vyakula vya jamii ya karanga au nuts kwa kiingereza vina faida kubwa kwa miili yetu. Vimejaa virutubisho na madini mbalimbali ambayo husaidia ufanyakazi bora wa mwili. Tafiti zimekuwa zikifanyika juu ya nuts, na tofauti na ilivyokuwa inafikiriwa zamani, tafiti zimeonesha faida nyingi zaidi za ulaji wa nuts.
Utafiti uliofanywa na madaktari katika kitengo cha Elimu ya Tiba katika chuo kikuu cha Harvard nchini Marekani kwa muda wa miaka 30, ulibainisha kuwa ulaji wa nuts mara 5 mpaka 7 kwa wiki hurefusha maisha kwa miaka 2 mpaka 3.
Sababu kuu ni kuwa nuts hupunguza hatari ya mtu kupata magonjwa ya kisukari, moyo, shinikizo la damu la kupanda na saratani ya utumbo. Magonjwa haya kwa kiasi fulani huchangiwa na sumu zinazijikusanya mwilini. Nuts zina virutubisho na madini ambayo hupunguza sumu mwilini ambazo huchangia kutokea kwa magonjwa haya.
Nuts zina mkusanyiko wa virutubisho vingi hasa ikiwa ni protini, wanga, mafuta ya omega-3, na omega -6, madini, vitamins na vitoa sumu mwilini (antioxidants) kama . Kuna nuts za aina mbalimbali, ambazo zipo kwa wingi hapa nchini ni karanga, korosho, ufuta, alizeti na almonds. Kuna aina nyingine za nuts kama chestnuts, hazelnuts, walnuts na pestachio ambazo huwa hazipatikani kwa wingi Afrika Mashariki, lakini unaweza kuzipata kwenye supermarkets mbalimbali.
Taasisi ya Chakula na Dawa (FDA) ya Marekani, inashauri ulaji wa nuts kwenye mlo kila siku kwa kiasi kisichopungua gramu 43 (ambayo ni sawa na karanga kwenye kiganja cha mkono).

0 comments:

Chapisha Maoni