Jumanne, Januari 19, 2016

UA LA KWANZA LAOTESHWA NJE YA DUNIA

 Wanaanga katika kituo cha kimataifa cha anga la juu, "International Space Station" hatimaye wamefaulu kukuza ua kwa mara ya kwanza nje ya dunia.
Skott Kelly, mwanaanga katika shirika la safari za anga la juu NASA, aliweka ujumbe wa picha katika mtandao wa Tweeter akionyesha ua aina ya 'zinnia' lililokuzwa kwenye maabara katika kituo hicho cha anga la juu.
Hapo mbeleni wanaanga wa NASA wamefaulu kukuza mimea kama ngano na mchicha kwenye maabara yao yaliyoko vituo hivyo.
Mwezi Agosti mwaka uliopita wanaanga wa NASA walikula, kwa mara ya kwanza, mchicha iliyokuzwa kwa maabara ndani ya vituo vya anga la juu. Mimea zaidi inatarajiwa kukuzwa kwenye vituo hivyo mwaka huu, ikiwemo kabeji ya kichina na mchicha, huku shirika hilo likijiandaa kupanda nyanya kwenye vituo vyake vya anga la juu ifikapo mwaka wa 2018.

0 comments:

Chapisha Maoni