Taarifa ambazo zimeifikia Fichuo muda mfupi uliopita kutoka eneo la Bonde la Mkwajuni, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ni kuwa barabara imefungwa kutokana na tukio la wananchi wa maeneo hayo kuchoma matairi na kujaza magogo barabarani.
Inadaiwa kuwa wananchi hawa ni wale waliovunjiwa nyumba zao kufuatia zoezi la bomoabomoa lililofanyika maeneo mbali mbali ya jiji hilo
, hivyo mpaka sasa hakuna mawasiliano ya Kinondoni na Magomeni kupitia ile barabara ya Kawawa kwani pamoja na hayo yanayofanyika, wananchi wanarushia mawe magari yanayopita maeneo hayo.
Tayari jeshi la polisi lilikwisha fika eneo hilo na kushughulikia hiyo shida.
0 comments:
Chapisha Maoni