Rais Dkt John Pombe Magufuli amewasimamisha kazi kamishna Jenerali wa uhamiaji Sylivester Mpukilwa na kamishna utawala na fedha Piniel Mgonja kupisha uchunguzi wa ukusanyaji maduhuli na uendeshaji wa idara hiyo.
Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue amesema katibu tawala aliyehamishwa Manyara kukaimu nafasi ya naibu kamishna wa mamlaka ya mapato TRA Eliachim Maswi amerejeshwa kwenye kazi yake ya katibu tawala Manyara baada ya kumaliza kazi aliyotumwa
0 comments:
Chapisha Maoni