Jumatano, Januari 13, 2016

KUKU ANYAKUA TSH. 2,435,000 ZA MGAO NA KUTOKOMEA NAZO MBEYA

Hii kali ya fungua mwaka imetokea Mbeya ambapo kuku amenyakua pesa za mgao wa kikundi walizoweka kwa mwaka mzima na kutoweka nazo, hii imetokea kwenye kikao cha mgao wa pesa za kikundi walizowekeza kwa mwaka mzima.
Wakiwa kwenye kikao hicho pesa yote inayofikia 2,435,000/= taslimu iliwekwa kwenye ungo huku pembeni nje ya kikao kukiwa na kuku mmoja akiwa katulia tuli muda wote.
Ghafla kabla mgao haujaanza lilipita wingu angani na yule kuku kwa kasi ya ajabu alichupa kwenye ungo na kunyakua Tsh 435,000/= taslimu na kutokomea  nazo kusikojulikana.
Hii yaweza kuwa mazingaombwe au uchawi lakini vyovyote iwavyo teknolojia ya uporaji inachukua sura mpya sasa.

0 comments:

Chapisha Maoni