Jumanne, Januari 19, 2016

KIKONGWE ZAIDI UINGEREZA ATIMIZA MIAKA 113

Mwanamke mkongwe zaidi nchini Uingereza aliyezaliwa wakati ndege ya kwanza ilipozinduliwa mwaka wa 1903 aliadhimisha miaka 113 jana (Jumatatu), huku akisema kuwa anajiskia mwenye nguvu kama mtu mwenye umri wa miaka 75!
Ajuza huyo kwa jina Gladys Hooper, ambaye hapo awali alikuwa mcheza piano, alisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kujiburidusha na chai kwa keki katika makazi ya wazee ya Isel of Wight katika eneo la Ryde anapoishi.
Alipoulizwa ikiwa angetaka kitu chochote, ajuza huo alijibu kwa kusema, "hapana, sidhani. Kwa kuwa nimeridhishwa na kila kitu na upendo kutoka kwa kila mtu."

0 comments:

Chapisha Maoni