Jumanne, Januari 05, 2016

BASI LA ABIRIA LASHIKA MOTO NA KUUA WATU 17

Watu 17 wamekufa na zaidi ya 32 kujeruhiwa baada ya basi ya abiria kushika moto (Jumanne asubuhi) katika mji wa Ningxia Hui, kaskazini magharibi ya China, taarifa kutoka kwa serikali imesema katika kile inashukiwa kuwa kitendo cha ugaidi.
Miongoni mwa waliofariki kwenye shambulizi hilo ni pamoja na wanaume nane na wanawake tisa.
Wote waliojeruhiwa kwenye shambulizi hilo wana umri wa kati ya miaka 20 na 65, na wanatibiwa katika hospitali ya chuo kikuu cha udaktari cha Ningxia, mjini Yinchuan, Ningxia.

0 comments:

Chapisha Maoni