Jumanne, Oktoba 28, 2014

MASHABIKI WAANZA KUREJESHA JEZI ZA BALOTELLI

Mashabiki wa Liverpool wameripotiwa kurudisha jezi za Mario Balotelli walizonunua baada ya staa huyo kujiunga na timu hiyo ili wapewe za mastaa wao makini baada ya Mtaliano huyo kuchemsha.
Mashabiki kadhaa walionekana wakipanga mstari na jezi zao zilizokuwa zimeandika ‘Balotelli 45’ mgongoni kuvua ili kupewa nyingine za mastraika waliofanya vizuri kwenye kikosi hicho kama Rush, Fowler na Owen.
Tukio hilo lilifanyika Jumamosi iliyopita kwenye mechi dhidi ya Hull City baada ya mashabiki hao kukerwa na kitendo cha Balotelli kubadilishana jezi na Pepe wa Real Madrid wakati wa mapumziko kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyomalizika kwa Liverpool kuchapwa mabao 3-0.

0 comments:

Chapisha Maoni