Afisa mmoja wa shirikisho la soka
nchini Uingereza FA amesimamishwa kazi kwa mda wa miezi minne baada ya
kumuambia refa mmoja wa kike kwamba anastahili kuwa jikoni badala ya
uwanjani.
Naibu raisi wa shirikisho la soka katika kaunti ya
Nothumberland John Cummings alitoa matamshi hayo kwa mkufunzi wa marefa
Lucy May katika mkutano wa marefa mnamo mwezi machi.
May mwenye
umri wa miaka 24 alimuuliza Cumminga kuhusu uwezekano wa kusimamia
katika ligi ya kazkazini mashariki siku ya jumapili.Lakini Cummings
alimwambia kwamba ataweza kulisimamia swala hilo.
Aliongezea
sikuingilii wewe lakini mda wote nitakao kuwa mzima,mwanamke hawezi kusimamia mechi katika ligi yangu
Baadaye tume huru ya shirikisho la
soka nchini humo iliamuru kwamba Cumminga ana hatia baada ya kukiuka
sheria za shirikisho hilo kupitia kutumia lugha chafu kwa lengo la
kudhalilisha jinsia nyengine.
Vilevile cummings amepigwa faini ya pauni 250 na ni sharti ahudhuri kikao cha mafunzoi kabla ya kuchukua tena wadhfa wake.
0 comments:
Chapisha Maoni