Jeshi la polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu wanne kutoka nchini Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila vibali.
Jeshi la polisi limewataja watu hao ambao walikamatwa jana saa 03:30 za usiku katika maeneo ya Uhindini na Ilomba kuwa ni pamoja na 1. Teshale Abebe (24), 2. Mohamed Taquand (34) 3. Akesh Juma (28) pamoja na 4. Mohammed Omari (32).
Baada ya jeshi la polisi kuwakamata watu hao, linafanya taratibu za kuwafikisha katika mamlaka husika ya Idara ya Uhamiaji kwa hatua nyingine stahiki za kisheria.
Baada ya jeshi la polisi kuwakamata watu hao, linafanya taratibu za kuwafikisha katika mamlaka husika ya Idara ya Uhamiaji kwa hatua nyingine stahiki za kisheria.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Kamkishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi amethibitishia Fichuo Tz juu ya kutokea kwa tukio hilo pia ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za watu wanaowatilia shaka katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na wahamiaji haramu ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe juu yao.

0 comments:
Chapisha Maoni