Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya linawashikilia watu sita ambao ni wahamiaji haramu kutoka nchi za Ethiopia na Burundi.
Kwa mujibu wa jeshi la polisi, watu hao waliokamatwa ni Zainab Asseta mwenye miaka 26 mkazi wa nchini Ethiopia, Kadeh Wahalu mwenye miaka 27 mkazi na raia wa Ethiopia, Jackquline Uhasi aliye na miaka 7 raia na mkazi wa nchini Burundi, na wengine waliofahamika kwa jina moja moja ni pamoja na Beathamwenye miaka 30 raia na mkazi wa nchini Burundi, Oliver aliye na miaka 25 mkazi na raia wa nchini Kongo na Davine mwenye miaka 25 raia na mkazi wa nchini Burundi.
Wahamiaji haramu hao wamekamatwa usiku wa kuamkia jana majira ya saa mbili na dakika hamsini katika kijiji cha Mkola wilayani Chunya mkoani hapa Mbeya.
Taarifa kutoka kwa jeshi la polisi mkoa wa Mbeya inasema kuwa wahamiaji hao walikamatwa wakati wakisafirishwa kwa basi lenye namba za usajili T.791 ACJ aina ya Scania mali ya kampuni ya Super Service na taratibu za kuwafikisha katika idara ya uhamiaji zinaendelea.
0 comments:
Chapisha Maoni