Siku kama ya leo miaka 60
iliyopita, mtetemeko mkubwa wa ardhi ulitokea katika eneo la
Orleansville kusini magharibi mwa Algeria. Janga hilo la mtetemeko wa
ardhi liliharibu kabisa mji mmoja uliokuwa na wakazi 30,000 na watu
10,000 wakapoteza maisha yao. Fauka ya hayo, makumi ya maelfu ya
wananchi wa kusini magharibi mwa Algeria walibaki bila ya makazi.
Mtetemeko huo pia ulitoa pigo kubwa kwa miundombinu ya uchumi wa nchi
hiyo.
Na miaka 100 iliyopita yaani
tarehe 10 Septemba mwaka 1914 kulitokea vita baina ya majeshi ya
Ujerumani na Russia kando kando ya ziwa la Mazury. Vita hivyo vilianza
kufuatia kuzuka Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia na kujiunga Russia na
kambi ya nchi Waitifaki. Katika vita hivyo vya Mazury, Wajerumani
wakiongozwa na kamanda Paul Von Hindenburg walipata ushindi na kuwauwa
takribani wanajeshi 20,000 wa Russia na kuwateka nyara wengine 45,000.
Hatimaye mwaka 1917 baada ya kutokea mapinduzi nchini Russia, nchi hiyo
ilijiondoa katika VitaVikuu vya Kwanza vya Dunia.




0 comments:
Chapisha Maoni