Siku kama ya leo miaka 278 iliyopita Daniel Gabriel Fahrenheit mwanahesabati na mwanafizikia wa Kijerumani aliyevumbua kipimajoto alifariki dunia akiwa na miaka 50. Fahrenheit alikuwa na fikra ya kubuni kifaa kitakachokuwa na uwezo wa kupima kiwango cha joto na ndipo mwaka 1724, msomi mwanafizikia huyo wa Kijerumani alipofanikiwa kutengeneza kipimajoto (thermometer). Kifaa hicho bado kinatumiwa hadi sasa na aina ya nyuzi joto za chombo hicho imepewa jina la msomi huyo mwenyewe yaani Fahreinheit. Daniel Gabriel Fahreinheit aliaga dunia mwaka 1686.
Miaka 83 iliyopita mwafaka na siku hii ya leo, aliuawa Omar al Mukhtar kiongozi wa taifa la Libya katika mapambano dhidi ya wakoloni wa Italia. Omar Mukhtar aliyekuwa kiongozi wa kidini alizaliwa mwaka 1859. Mwaka 1895 alielekea Sudan na kushiriki katika harakati za kupambana na ukoloni wa Uingereza. Baada ya kushindwa kwa harakati hizo Omar Mukhtar akalazimika kurejea nchini Libya. Mwaka 1911 Wataliano wakiwa na lengo la kuitawala Libya walianzisha vita na dola la Uthmania. Kiongozi huyo wa kidini aliwahimiza wapiganaji wa makabila ya Libya kusimama kidete na kupambana dhidi ya wavamizi wa Kitaliano. Hata hivyo kwa kutumia askari wengi zaidi na silaha za kisasa wavamizi hao wa Kitaliano walimzingira Omar Mukhtar na wenzake na kumkamata na kisha wakamnyonga katika siku kama ya leo.

0 comments:
Chapisha Maoni