Siku kama ya leo miaka 13 iliyopita Ahmad Shah Masoud mmoja wa makamanda wakubwa wa Mujahidina wa Afghanistan ambaye pia alikuwa Waziri wa Ulinzi katika serikali ya mpito ya Rais Burhanuddin Rabbani wa Afghanistan, aliuawa. Ahmad Shah Masoud alizaliwa mwaka 1952 na alianza kupigana vita na nchi za kigeni katika milima ya kaskazini mwa Afghanistan sambamba na kuingia madarakani wakomunisti nchini humo na baada ya hapo kukaliwa kwa mabavu nchi hiyo na jeshi la Urusi ya zamani mwaka 1979. Alikuwa kamanda hodari sana kiasi kwamba majeshi ya Urusi na hata wapiganaji wa kundi la Twaliban walishindwa kuteka eneo lililokuwa chini ya udhibiti wake katika bonde la Panjshir. Kwa sababu hiyo kamanda huyo shujaa alijulikana kwa jila la Simba wa Panjshir. Katika miaka ya mwishoni mwa umri wake Ahmad Shah aliongoza muungano uliokabiliana na wapiganaji wa Twaliban waliokuwa wakiungwa mkono na kusaidiwa na Marekani na Pakistan na kuwashinda mara kadhaa.
Siku kama ya leo miaka 927 iliyopita alizaliwa mjini Baghdad Iraq, Ibn Jawzi, mtaalamu wa fiq'hi na mtoa waadhi mashuhuri wa karne ya sita Hijria. Kwa muda mrefu wa uhai wake Ibn Jawzi alijishughulisha na kazi ya kutafuta elimu na kufahamiana na wasomi wakubwa wa zama zake katika safari alizozifanya katika miji mbalimbali. Ibn Jawzi alitambulika kwa kuwa na elimu kubwa na kupenda watu na aliheshimiwa na watu wote. Msomi huyo ameandika vitabu vingi vikiwemo vile vya "Al-Muntadhim", "Idhaahul-Qawaanin" na "Mawaaidhul-Muluuk". Ibn Jawzi alifariki dunia mwaka 597 Hijria.
Na siku kama ya leo miaka 1442 iliyopita kulianza vita maarufu kwa jina la vita vya miaka saba kati ya madola mawili yaliyokuwa na nguvu ya Iran na Roma, baada ya mfalme Justinian wa Roma kuanzisha mashambulizi yaliyokuwa na lengo la kulikalia eneo la magharibi mwa Iran. Baada ya miaka saba ya vita mfalme wa Iran Anushirvan alimshinda mfalme Justinian wa Roma na hivyo mfalme huyo akalazimika kujiuzulu. Baada ya kujiuzulu mfalme Justinian mfalme Tiberius alishika mamlaka ya utawala wa Roma. Vita hivyo vilimalizika mwaka 579 baada ya Waroma kukubali kuilipa Iran gharama inayofikia sarafu za dhahabu elfu 45.

0 comments:
Chapisha Maoni