Suarez, ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa kucheza soka kwa kipindi cha miezi minne, anatarajiwa kurejea uwanjani na kuanza kuitumikia FC Barcelona iliyomsajili wakati wa usajili wa majira ya kiangazi akitokea nchini Uingereza kwenye klabu ya Liverpool.
Ufafanuzi uliotolewa na mahakama ya usuluhisho kwenye msuala ya kimichezo CAS ambayo ilimpunguzia adhabu mshambuliaji huyo na kumuamuru kufanya mazoezi na kikosi cha FC Barcelona umeeleza kwamba Suarez atakuwa huru mara baada ya usiku wa Oktoba 24 mwaka huu.
Ufafanuzi huo unadhihirisha wazi kwamba Suarez huenda akawa sehemu ya kikosi cha FC Barcelona ambacho kitaikabili Real Madrid kwenye mchezo wa ligi ya nchini Hispania unaojulikana kwa jina la *El Clasico* ambao umepangwa kufanyika oktoba 25.
Hata hivyo shirikisho la soka nchini Hispania kupitia bodi inayosimamia ligi ya nchini humo LFP, linatarajiwa kutoa taarifa rasmi za kurejea kwa mshambuliaji huyo katika michezo ya kimashindano kati kati ya juma lijalo.
Kufuatia mwenendo wa suala hilo kuingia mkanganyiko, meneja wa FC Barcelona Luis Enrique Martínez García amesema anaamini mambo yote yatakwenda vizuri na atapata nafasi ya kumtumia Suarez ambaye anasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani kote kwa kuona anaitumikia Barca
Luis Alberto Suarez Diaz alikumbwa na rungu la adhabu kutoka FIFA baada ya kubainika alimng’ata begani kwa makusudi beki wa timu ya taifa ya Italia pamoja na klabu ya Juventus Giorgio Chiellini wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 ambazo ziliunguruma mwaka nchini Brazil.

0 comments:
Chapisha Maoni