Aina mpya ya Dinosaria imetambuliwa kufuatia kupatikana kwa mifupa nchini Tanzania.
Mabaki
hayo ya Dinosaria yaliyopewa jina la - 'Rukwatitan Bisepultus' -
yalipatikana katika korongo moja kwenye eneo la Rukwa, kusini magharibi
mwa nchi hiyo.
Inadhaniwa mnyama huyo aliyekuwa akiishi kwa kula
majani, aliishi karibu miaka mia moja iliyopita, na alikuwa na uzito
sawa na tembo kadhaa na alikuwa na miguu ya mbele yenye urefu wa mita
mbili.
Mnyama huyo ni aina ya Titanosaurus -- ambao ni wakubwa, na wanaokula nyasi.
Mabaki
ya wanyama aina hiyo mpaka sasa yamepatikana katika maeneo ya Amerika
ya Kusini, bara ambalo lilijitenga kutoka Afrika katika kipindi cha
Cretaceous, (kipindi ambacho miamba ya chokaa iliumbika) takriban miaka
milioni mia moja na arobaini iliyopita.





0 comments:
Chapisha Maoni