Ijumaa, Septemba 12, 2014

HUYU NDIO MTOTO WA MIAKA 11 ANAYETAKIWA CHELSEA

Klabu ya Chelsea imewasilisha ofa Camp Nou kwa ajili ya kutaka kumsajili mtoto mwenye umri wa miaka 11, Xavier Simons, gazeti la The Express la nchini Uingereza limeripoti mapema hii leo.
Gazeti la The Express, limeeleza kwamba Chelsea wamewasilisha ofa hiyo huku wakiamini watafanikiwa kumsajili kinda huyo kutoka nchini Uholanzi sanjari na kuwashawishi wazaizi wake ili iwe rahisi kumpata.
Ushawishi unaotarajiwa kufanywa na viongozi wa klabu hiyo ya magharibi mwa jijini London, ni kutaka kuihamishia familia ya mtoto huyo jijini London kama kigezo cha kuwa karibu na Xavier Simons.
Hata hivyo baadhi ya vyombo vya habari vya mjini Barcelona vinaripoti kwamba uongozi wa FC Barcelona umeikataa ofa ya Chelsea na umejipanga kuendelea kumkuza kijana huyo hadi kufikia hatua ya kucheza kwenye ngazi za juu.
Sababu kubwa inayotajwa na vyombo vya habari vya mjini Barcelona zinatuama kwenye adhabu ambayo iliiangukia klabu hiyo ya Catalan kutoka FIFA ya kufungiwa kusajili kwa kipindi cha misimu miwiwli mfululizo, hivyo wameona ni bora kuendelea kuwakuza vijana kupitia kituo wanachokimiliki *La Masia*.

0 comments:

Chapisha Maoni