Jumatatu, Septemba 15, 2014

HIVI NDIVYO BANGI INAVYOSUMBUA IRINGA

Watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Iringa kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bhangi.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema askari polisi doria wakiwa wamemkamata Ally Yusuph umri miaka 36 mkazi wa kijiji cha Kalenga wilaya ya Iringa Vijijini Mkoani Iringa akiwa na bhangi yenye uzito wa kilo 2.5 alizokuwa amezihifadhi nyumbani kwake baada ya kufanyiwa upekuzi.
Ameongeza kuwa huko katika maeneo ya bbarabara mbili kata ya Makorongoni Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa askari polisi wakiwa doria wamemkamata Godlove Clever 25 mkazi wa Makorongoni akiwa na bhangi kete ambapo mtuhumiwa ni muuuzaji na mtumiaji wa madawa hayo.
Kamanda Mungi amesema askali polisi wakiwa doria maeneo ya Ipogolo Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa wamewakamata Saidi Mohamed umri miaka 17 akiwa na bhangi kete 165,James John umri miaka 23 na Prince Mahundi umri miaka 21 wakiwa na bhangi yenye uzito wa gramu 200 ambapo uchunguzi wa awali umebaini kuwa watuhumiwa hao ni wauzaji na watumiaji wa madawa hayo.
Aidha amesema chanzo cha matukio hayo ni utafutaji wa kipato ambapo watuhumiwa wote wamekamatwa kwenye msako mkali uliofanywa Sept 14 mwaka huu na askari polisi wakiwa doria katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa na wilaya zake zote pia jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi wa matukio hayo ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani.
Hata hivyo Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Iringa kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za matukio ya kihalifu kwa wakati ili kuufanya Mkoa wa Iringa uwe katika hali ya usalama na amani.

0 comments:

Chapisha Maoni